Bwana Mungu nashangaa kabisa, Nikifikiri jinsi ulivyo, Nyota, ngurumo, vitu vyote pia, Viumbavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu, Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe ulivyo mkuu. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia. Nikikumbuka vile wewe Mungu, Ulivyompeleka mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno. Yesu Mwokozi atakaporudi, Kunichukua kwenda mbinguni, Nitaimba sifa zako milele, Wote wajue jinsi ulivyo. Mel : Sanningsvittnet 1891 [O STORE GUD] Text: Carl Gustaf Boberg 1886 "O store Gud" EN : Stuart Wesley Keene Hine 1949 "How Great Thou Art" Swahili: "Bwana Mungu nashangaa kabisa" Web : http://www.liederschatz.net