Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kukubali neno lake, Nina raha moyoni. Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti; Yesu,Yesu,yu thamani, Ahadi zake kweli. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake, Nimeoshwa kamili. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kwake daima Napata, Uzima na amani. Nafurahi kwa sababu, Nimekutegemea, Yesu,Mpendwa na Rafiki, Uwe nami dawamu. Mel : William James Kirkpatrick 1882 [TRUST IN JESUS] Text: Louisa M. R. Stead 1882 "'Tis So Sweet To Trust In Jesus" Swahili: "Kumtegemea Mwokozi" Web : http://www.liederschatz.net